Mawakibu za kuomboleza: Mwenyezi Mungu akuze malipo yako ewe Abulfadhil Abbasi

Maoni katika picha
Mawakibu za kuomboleza kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala zimemiminika katika malalo ya mbeba bendera ya Imamu Hussein (a.s) na mtoto wa Ummul-Banina (a.s) Abulfadhil Abbasi (a.s), kuja kumpa pole katika kumbukumbu ya kifo cha mama yake asubuhi ya leo siku ya Jumatatu (13 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (17 Januari 2022m), kama sehemu ya kuadhimisha alama za Mwenyezi Mungu na matukio ya Ahlulbait (a.s).

Matembezi ya mawakibu yamefanywa kwa kufuata ratiba maalum iliyopangwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu, kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Mawakibu zimebeba bendera za kuomboleza huku zikiimba kaswida za huzuni na majonzi, zilizojaa maelezo ya utukufu wa Ummul-Banina (a.s) na nafasi aliyopewa na Mwenyezi Mungu, (hakika alikua miongoni mwa wanawake waliotambua utukufu na haki ya Ahlulbait (a.s), aidha alikua mfasaha na mchamungu).

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya iliandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba wa kifo chake (a.s), yenye vipengele vingi sambamba na kupokea mawakibu na waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: