Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandika historia takatifu ya bibi Ummul-Banina -a.s- katika kumbukumbu ya kifo chake.
Majlisi ya kuomboleza imefanywa ndani ya ukumbi wa jengo la chuo na kuhudhuriwa na rais wa chuo na wajumbe wa kamati ya walimu na watumishi wake.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Sayyid Ahmadi Zamiliy kutoka Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, halafu Shekh Jafari Waailiy akapanda kwenye mimbari, akaongea kuhusu utukufu wake na nafasi yake katika jamii, na mwenendo wake (a.s) unaofaa kuigwa na kila mwanamke wa kiislamu, akaongea pia kuhusu maisha yake matukufu, na namna alivyo waliwaza Maimamu wa Ahlulbat (a.s), hakika alikua mliwazaji bora kwao ndio akapata hadhi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu hadi akawa miongoni mwa milango ya haja.
Pembezoni mwa tukio hilo ugawaji wa chakula ukafanyika kwa wanafunzi na watumishi wa chuo.
Kumbuka kuwa majlisi ni sehemu ya ratiba ya chuo kikuu cha Alkafeel katika kuhuisha kumbukumbu za Ahlulbait (a.s) na kubainisha nafasi ya Maasumina katika kujenga jamii ya kiislamu, kwa kukumbuka siku za kuzaliwa na kufariki kwao.