Idara ya shule za Dini Alkafeel za wasichana chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuendelea kwa maandalizi ya kufanya hafla ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq (awamu ya tatu ya mabinti wa Alkafeel), maandalizi hayo yameanza muda mrefu na yapo hatua za mwisho.
Hafla itafanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Kutokana na nuru ya Fatuma -a.s- dunia inamwanga), hafla hiyo itafanywa sambamba na kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (a.s), siku ya Ijumaa (28 Januari 2022m), kutakuwa na vipengele vingi vinavyo endana na wanafunzi wa chuo.
Kamati ya maandalizi imetoa wito wa kushiriki kwenye hafla hiyo, kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia namba zilizo andikwa kwenye vipeperushi.
Kumbuka kuwa shule za Dini Alkafeel hufanya harakati mbalimbali zinazo husu wanachuo wa kike, ikiwemo hafla hii itakayo fanywa kwa mwaka wa tatu mfululizo, na hupata muitikio mkubwa kutoka kwa wasichana wanaosoma kwenye vyuo vikuu mbalimbali.