Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi na wajumbe aliofuatana nao, wamempongeza katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya bwana Hassan Rashidi Al-Abaiji, kwa kuteuliwa kwake kuchukua madaraka hayo ya ukatibu mkuu.
Ugeni uliohusisha wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu na marais wa vitengo na wasaidizi wao, umewasilisha salamu na pongezi za kiongozi mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu wake mkuu, wamemtakia mafanikio mema katika kuhudumia malalo ya bwana wa vijana wa peponi Imamu Hussein (a.s) na mazuwaru wake.
Kikao kimeshuhudia maneno mazuri kutoka pande zote mbili na kuangalia namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Ataba mbili takatifu, pamoja na kuangalia namna ya kuboresha huduma kwa mazuwaru watukufu.
Kikao kikahitimishwa kwa kutoa zawadi kutoka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kumkabidhi bwana Abaiji, na kumuomba Mwenyezi Mungu amuwezeshe kutekeleza malengo yake.