Sayyid Swafi akutana na ugeni wa wasomaji wa Qur’ani wa kimataifa na apongeza juhudi zao katika kuhudumia kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu

Maoni katika picha
Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi amekutana na wasomaji wa Qur’ani wa kimataifa katika chuo kikuu cha Alkafeel, na washiriki wa kongamano la (mradi wa kuboresha mbao za Qur’ani) linaloratibiwa na Darul-Qur’anul-Kariim katika Atabatu Husseiniyya tukufu.

Ugeni huo umefuatana na rais wa Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya Dokta Ahmadi Sheikh Ali.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya amepongeza kazi kubwa inayofanywa na walimu wa Qur’ani rukufu, ya kufundisha kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu katika ulimwengu wa kiarabu na kiislamu pamoja na nchi zingine duniani.

Kikao hicho kimepambwa na ujumbe wa utambulisho uliotolewa na rais wa chuo cha Alkafeel Dokta Nurisi Dahani, ameeleza kwa ufupi kuhusu shughuli za chuo na mafanikio yake kielimu, kimajengo na kimaabara, sambamba na kuwa mwenyeji wa makongamano mbalimbali.

Ziara hii ni sehemu ya ratiba ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, sambamba na kuonyesha namna Ataba inavyo jali wanachuoni na watafiti, na kufungua milango ya mawasiliano kitaifa na kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: