Semina mpya za Qur’ani zinaendeshwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya semina nne mpya katika mkoa wa Najafu.

Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jawadi Aljaburi amesema: “Maahadi inafanya semina hizi kwa lengo la kupata idadi kubwa ya wasichana wenye uwezo wa kusoma Qur’ani kwa kufuata hukumu zake, sambamba na kufanyia kazi mafundisho ya kitabu kitakatifu”.

Akasema kuwa: “Semina hizi nne zinahusu hukumu za usomaji wa Qur’ani, semina hizo zimepewa majina yafuatayo (Ahbaabul-Hujjat, ya wasichana wa sekongari -upili-, Dhuha, Shamsu, ya wasichana wa shule za msingi na semina ya Haafidhwaati-Nuur, ya wasichana wa vyuo)”.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake ni moja ya vituo vya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, yenye jukumu la kufundisha Qur’ani na kuandaa jamii ya wanawake wasomi wa Qur’ani na wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta zote za Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: