Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil imeanza kutoa mitihani ya majaribio kwa washiriki wa mradi wa Haqibatul-Qur’aniyya

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil imeanza kutoa majaribio kwa wanafunzi wanao omba kushiriki kwenye mradi wa Haqibatul-Qur’aniyya katika mwaka 2022m.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil Sayyid Muntadhiru Mashaikhi amesema: “Haqibatul-Qur’aniyya ni miongoni mwa miradi muhimu inayo simamiwa na Maahadi, tumeweka mikakati kuhakikisha unakua na mafanikio tarajiwa”.

Akaongeza kuwa: “Usajili wa maombi ya kushiriki kwenye mradi huo, hadi sasa ni zaidi ya (375) kutoka sehemu tofauti za mkoa wa Baabil”.

Akabainisha kuwa: “Tunawapa mitihani ya majaribio kwa ajili ya kuwapanga kulingana na kiwango cha kila mshiriki, kwa baraka za bwana wa maji na ukarimu masomo ya hatua ya kwanza yataanza siku ya Ijumaa tarehe (21/01/2022m).

Tambua kuwa mradi wa Haqibatul-Qur’aniyya wa mwaka 2022m utaendelea kwa muda wa miaka miwili kamili, masomo yakafundishwa siku mbili kwa wiki.

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Baabil, hufanya harakati mbalimbali za Qur’ani, pamoja na kufanya semina endelevu hapa mkoani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: