Maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya Iraq katika zoezi linalo simamiwa na idara ya Qur’ani

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeshuhudia maelfu ya washiriki kutoka ndani na nje ya Iraq, katika zoezi la kusoma sura mbili (Alfaat-ha na Yaasiin) na kuzitoa zawadi kwa Ummul-Banina (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake.

Link ya kushiriki katika usomaji huo imefika kwenye nchi mbalimbali za kiarabu na kiajemi, kama vile Australia, Marekani, Uturuki, Norwey, Kanada na Ufaransa, pamoja na mikoa ya Iraq.

Washiriki wa zoezi hilo wamesifu kazi nzuri zinazofanywa na idara ya Qur’ani zenye faida kielimu na kiroho kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) duniani kote.

Zowezi hili limefanywa kwa kuzingatia kuwa Ummul-Banina (a.s) ni shule, lazima tujifunze kutoka kwake na tumfanye kuwa mfano mwema wa kuigwa katika maisha yetu.

Kumbuka kuwa idara ya Qur’ani chini ya ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya, hufanya harakati mbalimbali zinazo husu Qur’ani katika kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: