Idara ya malezi ya Baabil inaangalia njia za kuimarisha ushirikiano wake na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa wakufunzi, viongozi wa idara na wanafunzi wake, ili kuboresha mazingira ya kielimu na kimalezi.
Hayo yamesemwa katika ziara iliyofanywa na ugeni kutoka idara ya malezi ya mkoa wa Baabil, iliyo ongozwa na mkuu wa idara hiyo Ustadh Mahadi Al-Awadi akiwa pamoja na jopo la watumishi wa idara hiyo na viongozi wa ofisi za malezi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Wamepokewa na makamo rais wa kitengo cha uhusiano cha Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Jalukhani na kiongozi wa idara ya uhusiano ya chuo, na viongozi wa kitengo, pamoja na kiongozi wa idara ya shule.
Kiongozi wa idara ya mahusiano ya vyuo na shule Ustadh Maahir Khalidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ujio wa ugeni huu umetokana na mahusiano mazuri yaliyo tengenezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu na idara za malezi kwenye mikoa tofauti, mahusiano hayo ndio chachu ya kufanyika kwa harakati tofauti katika shughuli ya malezi na elimu, miongoni mwa idara ambazo tunauhusiano mzuri ni hii ya mkoa wa Baabil, ambayo imekua ikivuna matunda ya ushirikiano.
Akaongeza kuwa: “Ziara imefanywa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na idara za malezi za Iraq, ziara imekua na matokeo chanya, idara ya malezi imeahidi kuandaa mashindano, safari na zielimu na mapumziko, pamoja na kuongeza wanufaika wa program zake, mwisho wakasaini mkataba wa ushirikiano baina yao kwa lengo la kuboresha sekta ya malezi na elimu, na kunufaika na uzowefu wa Atabatu Abbasiyya katika sekta hiyo”.
Ugeni huo ukahitimisha ratiba yao kwa kufanya ziara na kusoma dua mbele ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha wakaagwa kama walivyo pokewa, wamesifu na kushukuru mapokezi mazuri waliyopewa na wahudumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.