Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na makamo wake wanakagua baadhi ya program za Qur’ani

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Dhiyaau-Dini na makamo wake Mhandisi Abbasi Mussawi wametembelea semina ya madhumuni ya Qur’ani katika Nahaju-Balagha na mradi wa Qur’ani wa kitaifa Alkafeel, inayofanywa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Ataba tukufu.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani Shekhe Jawadi Nasrawi amesema: “Maahadi inathamini sana ziara hii, ambayo ni miongezi mwa utendaji wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kusaidia sekta ya Qur’ani na kuhakikisha inaendelea vizuri, sambamba na kushajihisha wahudumu wa sekta hiyo kufanya kila wawezalo katika kutumikia vizito viwili vitakatifu”.

Akasisitiza kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu husimamia miradi mingi ya Qur’ani, shughuli zinazo husu Qur’ani ni miongoni mwa vipaombele vyake, jambo hili limeshuhudiwa katika miaka yote na bado linaendelea, hakika limekua likitusukuma kufanya kazi kwa bidii katika sekta hii takatifu”.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya vituo vya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kufundisha Qur’ani na kuchangia katika kuandaa jamii yenye kufanyia kazi mafundisho ya Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: