Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imepokea barozi wa muungano wa Ulaya nchini Iraq Mheshimwa Filah Faryula, rais wa makumbusho Ustadh Swadiq Laazim Zaidi na rais wa kitengo cha mahusiano Ustadh Muhammad Ali Azhar wameongoza mapokezi hayo.
Zaidi ametoa maelezo kwa ujumla kuhusu makumbusho na malikale zake, kisha barori akatembezwa ndani ya makumbusho hiyo na kuonyeshwa vitu tofauti, pamoja na kusikiliza ufafanuzi wa malikale mbalimbali zilizopo kwenye makumbusho hiyo na namna zinavyo tunzwa.
Barozi ameonyesha kufurahishwa kwake, kwa kutembelea makumbusho hiyo na kuona malikale adimu zinazo wakilisha turathi mbalimbali, aidha amepongeza utaratibu mzuri unaotumika katika kuonyesha malikale hizo, akashukuru sana kupewa nafasi ya kutembelea makumbusho hiyo.
Kumbuka kuwa makumbusho ya Alkafeel hutembelewa na wageni mbalimbali wanao wakilisha taasisi za makumbusho na za kielimu, pamoja na viongozi wa kitaifa na kimataifa kutoka ndani na nje ya Iraq, kutokana na malikale adumu ilizonazo.