Uongozi wa chuo kikuu cha Al-Ameed umekamilisha maandalizi ya kuteua wanafunzi wapya waliohitimu kozi ya uuguzi awamu ya kwanza, katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mji wa Karbala, kama sehemu ya kuthamini juhudi walizo onyesha wakati wa masomo, sambamba na kunufaika na wahitimu wa chuo kwa kuwapa nafasi ya kufanyia kazi kwa vitendo yale waliyofundishwa darasani.
Kikao cha uteuzi kimehusisha mkuu wa hospitali Dokta Jaasim Ibrahimi na wahitimu, amewakaribisha na kuwatakia mafanikio katika kazi zao, amewataka wafanyie kazi kwa vitendo ujuzi waliofundishwa wakati wa masomo yao katika chuo kikuu cha Al-Ameed, akawaambia kuwa moja ya mahitaji muhimu kwa wale walioteuliwa na kupangiwa majukumu ni kuendelea kushiriki katika mihadhara, warsha, nadwa na semina mbalimbali, pamoja na kuweka utaratibu wa maisha yao, na mambo mengine ambayo ni muhimu kwao.
Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed huchukua wanafunzi wanaopata nafasi za kwanza kwenye masomo yao katika kitivo cha (Udaktari – Uuguzi – Udaktari wa meno) chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu na uongozi mkuu, kwa lengo la kunufaika na uwezo wa raia wa Iraq, na kuhakikisha wanaendelea kujengewa uwezo.