Maktaba (84) za umma na binafsi pamoja na waandishi (178) wa mkoa wa Dhiqaar na vitabu vyao, wameingizwa kwenye mradi wa faili rejea, ambao ni moja ya miradi ya kituo cha faharasi na kupangilia taaluma katika maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya chini ya kitengo cha habari na utamaduni, tumekamilisha kuingiza taarifa kwenye toghuti ya mradi http://afiqa.net ili baadae ziingizwe taarifa za mikoa mingine, zitaongezwa taarifa za maktaba na waandishi wengine wa kiiraq.
Mradi unatoa huduma bure, unahusisha taarifa za waandishi wa kiiraq na kila kitu kinacho husu vitabu vyao na historia zao, pamoja na aina zote za maktaba na kuweka mikakati ya kuzitunza, sambamba na kurahisisha utambuzi wa sehemu zilipo na vitavu vilivyo andikwa na raia wa Iraq kama sehemu ya kuenzi juhudi za waandishi hao.
Faili rejea ndio njia ya kimataifa linayotumiwa na nchi nyingi zilizo endelea, nalo ni faili ya kwanza kuandaliwa kwa njia ya mtandao katika nchi za kiarabu, kituo na watumishi wake wanafanya kazi kubwa ya kuingiza idadi kubwa ya maktaba na waandishi wa kiiraq kwenye faili hilo.
Kumbuka kuwa faili rejea la waandishi wa kiiraq, linamilango mingi inayotambulisha maktaba mbalimbali za Iraq, aidha tunatoa wito kwa kila muandishi wa kiiraq atume jina lake na taarifa zake kwenye link ifuatayo (http://afiqa.net) ili aingizwe bure kwenye faili rejea.