Kukamilika maandalizi ya kongamano la kukumbuka mazazi ya bibi Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamekamilisha maandalizi ya kongamano la kwanza la kukumbuka mazazi ya mbora wa wanawake duniani bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Linalo tarajiwa kufanywa wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, saa tatu na nusu asubuhi siku ya Jumatatu, mwezi ishirini Jamadal-Aakhar sawa na tarehe (24 Januari 2022m) ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s).

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo na kiongozi wa maktaba ya Ummul-Banina (a.s) bibi Asmaa Ra’ad amesema: “Watumishi wa tawi la wanawake wamefanya maandalizi kamili na kuweka ratiba maalum inayo onyesha wajibu wa kila idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ratiba hiyo inahusisha redio ya Alkafeel, idara ya maelekezo ya kidini na maktaba ya Ummul-Banina (a.s) na idara ya Zainabiyyaat, ambayo imezowea kutoa huduma kwa ajili ya mbora wa wanawake (a.s), nayo ni sehemu ya harakati za idara katika kuhudumia jamii na kufundisha Dini kwa wanawake, sambamba na kubainisha mafundisho ya Zaharaa (a.s) katika umma wa kiislamu kuanzia zama zake hadi sasa”.

Akaongeza kuwa: “Kongamano litakua na vipengele vingi pamoja na mashindano ya aina mbalimbali, mambo yote yatakayo fanyika yanahusiana na bibi Zaharaa (a.s), yanalenga kuonyesha utukufu wake na kujifunza kitu katika historia yake”.

Kamati ya maandalizi imetoa wito kwa wasomi na watafiti wa kike kuja kushiriki kwenye kongamano hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: