Atabatu Abbasiyya tukufu inapokea mazazi ya Zaharaa (a.s) kwa mapambo mazuri na muonekano wa furaha

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inapokea kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Fatuma Zaharaa mtoto wa Mtume na tulizo la jicho la mtukufu Muhammad (s.a.w.w), aliyezaliwa sawa na tarehe ya Jumatatu (mwezi 20 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (24 Januari 2022m), kwa muonekano wa furaha na mapambo yamewekwa kila sehemu ndani ya malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Vitengo vinavyo husika katika Ataba tukufu, vimepamba vizuri ukumbi wa haram, na kuufanya uendane na mazingira ya maadhimisho hayo, hakika nuru ya kuzaliwa kwake (a.s) iliangaza ardhi na mbingu na viumbe wote waliomo miongoni mwa Malaika, majini na binaadamu walifurahi.

Ukumbi wa malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na korido zake zinawakawaka, kunamabango yaliyo dariziwa maneno mazuri ya pongezi za kuzaliwa mbora wa wanawake, aidha mauwa yamewekwa ndani na nje ya haram tukufu, na zimewashwa taa za rangi, kama alama ya maadhimisho hayo matukufu, na kuingiza furaha katika nyoyo za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) watakaokuja kuadhimisha mazazi hayo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Atabatu Abbasiyya tukufu imejiandaa kupokea mazuwaru watakao kuja katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kutoa pongezi zao kwa tukio hili tukufu, sambamba na hilo Ataba imeandaa ratiba maalum ya kuhuisha tukio hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: