Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, linafanya kongamano la kuzaliwa tunda la peponi Fatuma Zaharaa (a.s), asubuhi ya leo mwezi (20 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (24 Januari 2022m) ndani ya ukumbi mkuu wa Maahadi, tamasha hilo limehudhuriwa na watumishi wa Maahadi, wanafunzi na wageni waalikwa.
Tamasha limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo fuatiwa na mawaidha kutoka kwa bibi Naqaa Hassan, amefafanua kuhusu maadhimisho haya matukufu na kahimiza umuhimu wa kufuata nyayo za bibi Fatuma Zaharaa (a.s), na kuhuisha ahadi ya kufuata mwenendo wake katika kila sekta ya maisha yetu, yeye ni kigezo chema kwa kila mwanamke wa kiislamu katika tabia yake, Maisha yake, elimu yake na Dini yake, akahimiza kunufaika na historia yake takatifu, akataja baadhi ya mambo binafsi aliyokua nayo mbora wa wanawake wa duniani, kila mwanamke wa leo anatakiwa kuishi kwa kufuata muongozo wa Zaharaa (a.s).
Katika tamasha hilo kulikua na igizo lililofanywa na wanafunzi, pamoja na kaswida na mashairi ya kumsifu.
Kumbuka kuwa tamasha hili ni sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mama huyu mtakatifu na kujifunza mwenendo wake mtukufu unaofaa kuigwa katika kila zama, hakika yeye ni kigezo chema kwa wanawake na wanaume.