Atabatu Abbasiyya inaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa wanawake (a.s)

Maoni katika picha
Ratiba ya maadhimisho iliyoandaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa wanawake duniani Fatuma Zaharaa (a.s) imehusisha vitu vingi.

Ikiwa ni pamoja na kufanya hafla ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya chini ya usimamizi wa kitengo cha mahusiano.

Hafla hiyo imehudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi wa malalo takatifu, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha zikasomwa tenzi na mashairi ya kuonyesha mapenzi kwa bibi Zaharaa (a.s), waliosoma tenzi hizo ni Ali Asili Al-Aamiliy, Zainul-Aabidina Saidi, Sayyid Badri Mamitha, Muslim Shabaki na Muhammad Tamimi, beti zao zilikua na maneno matam yaliyoburidisha masikio ya wahudhuriaji, katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa wanawake Fatuma Zaharaa (a.s).

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imesha andaa ratiba maalum ya kupokea mazuwaru wanaokuja katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kumpongeza kwa tukio hili tukufu kwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao, sambamba na hilo Atabatu Abbasiyya imeandaa utaratibu maalum wa kuadhimisha tukio hili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: