Wito wa kuhudhuria na kushiriki katika nadwa ya kielimu kuhusu misingi ya kutunza malikale za makumbusho

Maoni katika picha
Makumbusho ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa wito kwa wasomi wote na wadau wa makumbusho wa kuhudhuria na kushiriki kwenye nadwa ya pili miongoni mwa nadwa za kitamaduni, itakayo fanywa chini ya anuani isemayo: (Misingi ya kielimu katika kutunza malikale za makumbusho).

Nadwa itafanywa saa nne asubuhi siku ya Jumamosi ya tarehe (29 Januari 2022m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya chini ya uhadhiri wa Ustadh Muhammad Qassim Muammaar kutoka kamati kuu ya athari na turathi katika wizara ya utamaduni na utalii.

Unaweza kushiriki na kufuatilia nadwa hiyo kwa njia ya mtandao kupitia (ZOOM) kwa link: https://us02web.zoom.us/j/3740873005

Password=1

Tambua kuwa kutakua na vyeti vya ushiriki vitatumwa kwenye barua pepe za washiriki baada ya nadwa.

Kumbuka nadwa hii inatokana na moja ya maazimio ya kongamano la makumbusho ya Alkafeel la kimataifa awamu ya tatu, iliyo sisitiza umuhimu wa makumbusho, kwa lengo la kulinda turathi zetu na utambulisho wetu wa kiarabu pamoja na lugha yetu na kupambana na hatari zinazo tuzunguka na kushambulia turathi zetu, nadwa hizi zitatukumbusha na kuibua mambo ambayo hayakuzungumzwa kwenye kongamano kwa lengo la kulinda na kutunza turathi za kihisia au kushikika, zilizopo kwenye makumbusho ya Alkafeel au sehemu nyingine yayote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: