Chuo kikuu cha Alkafeel kinaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa mbora wa wanawake kwa kusoma Qur’ani na kutoa zawadi kwa wanafunzi waliovaa Abaa za Fatwimiyya

Maoni katika picha
Chuo kikuu chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa wanawake Zaharaa (a.s), kwa kufanya kikao cha kusoma Qur’ani chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatuma Zaharaa ni mto na taa la uongofu na mwanga).

Siku ya Jumatatu mwezi (20 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (24 Januari 1443h), mbele ya rais wa chuo Dokta Nurisi Dahani na viongozi wa vitivo, wakufunzi, wanafunzi, na wageni wanaowakilisha watu wa makundi tofauti.

Maadhimisho ya kumbukumbu hii hufanywa kila mwaka, na huwa kuna vipengele tofauti, kikiwemo cha usomaji wa Qur’ani unaofanywa kwa kushirikiana na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu, chini ya Majmaa ya Qur’ani ya Atabatu Abbasiyya.

Hali kadhalika maadhimisho hayo yamepambwa na ujumbe kutoka kwa rais wa chuo, ametoa pongezi za dhati kwa washiriki wa maadhimisho haya, akafafanua kuwa “Chuo kikuu kinafanya kila kiwezalo katika kuhakikisha kinafuata mwenendo wa kiislamu na kufanyia kazi maelekezo yote ya kimaadili”, mwisho akatoa shukrani za dhati kwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu na katibu wake mkuu, kwa kusaidia miradi ya elimu na malezi, akawashukuru wanafunzi kwa kumuiga bibi Zaharaa (a.s) ambaye ni kilele cha kujihifadhi na haya.

Hafla imepambwa na kaswida na mashairi yenye beti zinazo zungumzia tukio hilo takatifu, mwisho wa hafla wanafunzi wanaozingatia hijabu (Abaa) kutoka katika vitivo na vitengo vya kielimu, wakapewa zawadi. Wao na familia zao wameshukuru sana kwa tukio hili, wamesema kua tukio hili limewatia hamasa zaidi watoto wao ya kuendelea kuvaa Abaa na kusoma hadi ngazi za juu kabisa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: