Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limefanikiwa kurudisha mapigo ya moyo katika hali ya kawaida kwa mtoto mwenye umri wa miaka (3) aliyekua na tatizo la mapigo ya moyo.
Daktari bingwa wa moyo kwa Watoto katika hospitali ya Alkafeel Dokta Ahmadi Abudi, amesema kuwa: “Jopo la madaktari wetu limefanikiwa kufanya upasuaji kwa mtoto mwenye umri wa miaka mitatu, aliyekua na tatizo la mapigo ya moyo tangu wakati wa kuzaliwa kwake”. Akabainisha kuwa: “Alikua na tatizo kubwa ambalo ilikua lazima afanyiwe upasuaji”.
Akafafanua kuwa: “Madaktari na wauguzi wa kitengo cha moyo, wanauzowefu mkubwa wa maradhi hayo, wanaweledi mkubwa wa kuhudumia mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo sawa awe mtoto au mkubwa”. Tambua kuwa: “Upasuaji wa aina hii ulikua unafanywa nje ya nchi, lakini baada ya kufunguliwa kituo hiki, unafanyika hapa nchini tena kwa mafanikio makubwa”.
Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.
Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali tofauti za maradhi yao.