Idara ya usomaji wa Qur’ani tukufu chini ya Maahadi ya Qur’ani katika Majmaa ya Qur’ani inafanya semina ya kuhakiki mahadhi ya Iraq na Misri, kwa ushiriki wa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Semina imehusisha masomo ya hukumu za tajwidi, matamshi ya herufi, sauti na naghma kwa mahadhi ya kiiraq na kimisri, chini ya ukufunzi wa Ustadh Alaau-Dini Hamudi Alhamiri na Sayyid Haidari Jalukhani, washiriki wapo zaidi ya (20).
Washiriki wameshukuru Atabatu Abbasiyya na Maahadi ya Qur’ani pamoja na walimu kwa juhudi kubwa wanayofanya ya kufundisha kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.
Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inajukumu la kufundisha Qur’ani tukufu na kuandaa jamii ya wasomi wa Qur’ani kwenye nyanja zote.