Wanafunzi wa shule za Al-Ameed wanampongeza Imamu Hussein katika kumbukumbu ya kuzaliwa mama yake Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya michezo ya Watoto katika shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein (a.s) kwa ajili ya kumpongeza kwa kumbukumbu ya kuzaliwa mama yake Zaharaa (a.s) na Mtoto wa mbora wa Mitume, bado tunaishi katika mazingira ya kumbukumbu hiyo takatifu.

Tukio hili linalenga kuonyesha utukufu wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) katika nafsi za Watoto hao.

Ziara imepambwa na harakati mbalimbali na usomaji wa kaswida zinazotaja utukufu wa Fatuma Zaharaa (a.s) aliyejitolea uhai wake kwa ajili ya Dini tukufu aliyokuja nayo Mtume Muhammad (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watakatifu (a.s).

Hali kadhalika ziara imepambwa na tendo la wanafunzi hao kugawa zawadi na maua kwa mazuwaru watukufu, kama ishara ya kuonyesha mapenzi yao na furaha yao katika tukio hili tukufu.

Kumbuka kuwa shule za Al-Ameed zinaharakati nyingi zinazo saidia kazi ya malezi na ufundishaji, ikiwa ni pamoja na kuadhimisha tarehe za kuzaliwa Maimamu watakasifu na kuomboleza tarehe za vifo vyao (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: