Kwa picha: Mikono ya watumishi wa msimamizi wake imemaliza hatua za mwanzo katika utengenezaji wa dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) limeshuhudia hatua za utengenezaji na uonganishaji wa vipande vyake kwa haraka, sura ya mwisho inaanza kuonekana siku baada ya siku kutokana na kazi ya mikono ya watumishi wa msimamizi wake, wanaofanya kazi katika kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya makaburi na milango mitukufu katika Atabatu Abbasiyya.

Tayali sura ya muonekano wa kwanza wa dirisha hilo imeonekana, baada ya kukamilika sehemu kubwa ya utengenezaji wa vipande vyenye madini na kuviunganisha kwenye umbo la mbao, kazi yote inafanywa na watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wana shauku kubwa ya kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa, wanafanya kazi kwa zaidi ya saa (12) kila siku, hadi hapo walipo fikia kwa sasa.

Rais wa kitengo na msimamizi mkuu wa kazi hiyo Sayyid Nadhim Ghurabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mafundi wetu wanaofanya kazi katika mradi huu, wamekamilisha sehemu kubwa ya kazi kuanzia sehemu ya vipande vinavyowekwa madini au sehemu ya vipande vya mbao, na vimesha unganishwa kwenye umbo la mbao, na leo sehemu nyingine imekamilishwa na kuunganishwa kwenye dirisha”.

Akaongeza kuwa: “Tumeanza kuonganisha sehemu nyingi za vipande vilivyo wekwa madini, kuanzia sehemu ya juu ambayo inamaandishi ya Qur’ani na mapambo, hadi kwenye vyumba vya madirisha na viunganishi vyake na nakshi zinazo zunguka dirisha, pamoja na ufito wa fedha, kazi hiyo imeleta muonekano wa picha ya dirisha”.

Akasisitiza kuwa: “Kazi iliyobaki inaendelea kama ilivyo pangwa, sasa hivi zinatendenezwa nguzo kuu ambazo ni sehemu muhimu inayo hitaji umakini mkubwa, pamoja na mapambo yaliyobaki yanayo pendezesha muonekano wa dirisha, hali kadhalika tumeanza kutengeneza mlango”.

Kumbuka kuwa kazi inaenda vizuri tena kwa umakini mkubwa katika kila sehemu, kama ilivyo pangwa na kupasishwa na wasimamizi wa mradi huu, mafanikio yataendelea kushuhudiwa katika kila sehemu inayotengenezwa kwenye dirisha hili jipya, umakini na weledi mkubwa unashuhudiwa katika utendaji wa kazi hii tukufu, hakika ufanisi wa mafundi katika utendaji wao ni mkubwa, mafanikio yao sio faida kwa Iraq pekeyake bali kwa nchi zote zinazo thamini utengenezaji wa madirisha ya kuweka kwenye makaburi matukufu, hiki ni kielelezo cha ufanisi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: