Kukamilika kwa semina ya khutuma na maandiko rasmi ya kiofisi

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimehitimisha semina inayohusu khutuba na maandiko maalum ya kiofisi kwa watumishi wake, ili kuwajengea uwezo wa utendaji wa shughuli za kiofisi, na kufahamu mambo ya msingi katika maandiko rasmi, pamoja na uandishi wa nyaraka za kiofisi kwa kuwapa mbinu za kisasa katika swala hilo.

Hii ni moja ya semina nyingi zinazo tolewa na kitengo hiki kwa watumishi wa vitengo tofauti katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya utaratibu maalum ulioandaliwa, wamefundishwa namna ya kuandaa khutuba za kiofishi na namna ya kuandika nyaraka maalum za ofiri sambamba na kubainisha makosa ya kilugha ambayo watu wengi huyafanya.

Semina hii imekua na washiriki (24), imedumu kwa muda wa siku tatu, ambapo wamesoma saa tatu kila siku, wamefundishwa mambo mengi, miongoni mwa waliyofundishwa ni: “Sifa za msingi za nyaraka rasmi, wamesoma kwa nadhariyya na vitendo kila siku, wakahitimisha kwa kufanya mtihani kwa ajili ya kupima kiwango cha uelewa wa washiriki na mafanikio yaliyopatikana katika semina hii”.

Tambua kuwa vitengo vilivyo shiriki kwenye semina hii ni (kitengo cha kulinda nidhamu, mahusiano, Majmaa ya Qur’ani tukufu, uboreshaji na maendeleo endelevu) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: