Taasisi ya Alfadhil ya kulea mayatima inaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa usimamizi wake wa karibu

Maoni katika picha
Taasisi ya Alfadhil ya kulea Watoto yatima ambayo makao makuu yake yapo Najafu, na inalea mamia ya Watoto yatima, inaushukuru uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa misaada mbalimbali unaotoa kwa Watoto hao.

Shukrani hizo zimewasilishwa katika ziara iliyofanywa na kiongozi wa taasisi hiyo Shekh Hussein Turabi, na akakutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini, na kukabidhi ngao ya taasisi kama sehemu ya kuonyesha thamani ya msaada wa Ataba tukufu kwa mayatima, hakika Atabatu Abbasiyya tukufu imekua ikisaidia bila kusimama, kupitia kiongozi wake mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi.

Kiongozi wa taasisi hiyo na ujumbe aliofuatana nao, wametoa pongezi kwa katibu mkuu mpya wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Dhiyaau-Dini kwa kupewa madaraka hayo matukufu, wakamtakia kazi njema na mafanikio katika kutumikia malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake watukufu.

Shekh Turabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Taasisi ipo huru na wala sio ya kibiashara, inahudumia mayatima wa mashahidi na Watoto waliofiwa na wazazi wao, kupitia program ya (Alkafeel baba yangu.. tunatoa chakula, matibabu na mavazi), pamoja na huduma zingine za kibinaadamu ikiwa ni sambamba na elimu, tunalea mayatima wa jinsia zote mbili hadi wanafika umri wa kubalekhe, aidha tunahudumia familia za mafakiri kwa kuwapa misaada ya aina tofauti, yote hayo tunayafanya kutokana na msaada mukubwa tunaopewa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Kumbuka kuwa miongoni mwa makundi ambayo Atabatu Abbasiyya inayapa umuhimu mkubwa ni kundi la mayatima, hususan mayatima wa mashahidi wa fatwa tukufu ya kujilinda, imekua ikiwasaidia moja kwa moja au kwa kutumia taasisi za kulea mayatima, na taasisi ya Alfadhil iliyopo katika mji wa Najafu na kulea mamia ya mayatima ni miongoni mwa taasisi hizo
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: