Kutoa uvimbe kwenye koo la mgonjwa kwa kutumia teknolojia ya mionzi

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limetangaza kufanikiwa kutoa uvimbe kwenye koo la mgonjwa mwenye umri wa miaka zaidi ya hamsini kwa kutumia teknolojia ya mionzi.

Daktari bingwa wa pua, sikio na koo katika hospitali hiyo, Dokta Nadhim Amrani amesema: “Hivi karibuni tumefanikiwa kutoa uvimbe kwenye koo ya mgonjwa kutoka mkoa wa Dhiqaar mwenye umri wa miaka (54)”, akasema: “Tumefanikisha matibabu hayo kwa kutumia teknolojia ya mionzi”.

Akafafanua kuwa: “Teknolojia ya mionzi inatuwezesha kuondoa uvime wa mgongwa bila upasuaji, na inatuepusha na madhara mengi yanayo weza kutokea wakati wa upasuaji”, akasema: “Uwepo wa vifaa-tiba vya kisasa katika hospitali ya rufaa Alkafeel sambamba na maabara ya kisasa inayotoa majibu kwa haraka ni sababu kubwa ya mafanikio yanayo shuhudiwa”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: