Alimu mkubwa Asadu-Llahi Kadhimiy.. historia yake na athari zake zinachunguzwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu

Maoni katika picha
Idara ya kutunza maarifa chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, siku ya Alkhamisi (23 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (17/1/2022m) imefanya nadwa yenye anuani isemayo: (Aalimu mkubwa Asadu-Llahi Kadhimiy.. historia yake na athari zake).

Nadwa imefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Qassim (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, mbele ya viongozi wa hauza, walimu, watafiti na wanahistoria.

Mtoa mada wa nadwa alikua ni Mhakiki Sayyid Osama Sharifi, ameongea kwa undani kuhusu hatua muhimu za Maisha yake, akaeleza historia ya kuzaliwa na kufa kwake, akafafanua kwa kutumia shuhuda mbalimbali, akataja vitabu alivyo andika na walimu wake pamoja na wanachuoni wa zama zake, akafafanua kuwa Shekhe Kadhimiy alikua na uwezo mkubwa wa akili na mwepesi wa kuhifadhi, baada ya hapo wahudhuriaji wakaanza kuuliza maswali, naye akajibu na kufafanua palipo hitaji ufafanuzi zaidi.

Baada yake akapanda kwenye mimbari Shekh Jihadi Asadiy, ambaye ni mjukuu wa Shekh Asadu-Llahi Kadhimiy, akaongea kwa ufupi kuhusu baadhi ya mambo yanayo husiana na Shekh Kadhimiy, akapongeza kazi nzuri inayofanywa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kubinaadamu ya kuhuisha turathi za kiislamu, akaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kusimamia nadwa hii inayo mzungumzia mwanachuoni huyu mtukufu.

Naye rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu Shekh Ammaar Hilali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni miongoni mwa nadwa muhimu, kwani tunazungumzia wanachuoni wakubwa walio acha urithi mkubwa ambao lazima tuutukuze na kunufaika nao, kwa kuwafundisha wanafunzi wa Dini na watafiti, tutaendelea kufanya nadwa kama hii kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Insha-allah, ili tuendelee kunufaika zaidi na wanachuoni hawa watukufu.

Wahudhuriaji wote wamesifu nadwa hii, wamepongeza anuani yake na madhumuni pamoja na uwasilishwaji wa mada, wamewashukuru wasimamizi wa nadwa na kuomba kufanyika kwa nadwa zingine sawa na hii.

Kumbuka kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu tangu kuanzishwa kwake, kimekua kikifanya nadwa na makongamano ya kueleza turathi kwa lengo la kuhuisha turathi za kiislamu, na kuonyesha umuhimu wake katika uwanja wa elimu na utamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: