Uwanja wa mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya leo siku ya Ijumaa mwezi (24 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (28 Januari 2022m) umefurika wahitimu wa vyuo vikuu waliomaliza mwaka jana (kundi la mabinti wa Alkafeel awamu ya tatu).
Hii ni hafla kubwa ya wahitimu wa kiiraq wa vyuo vikuu kuandaliwa na idara ya shule za Alkafeel za Dini tawi la wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kauli mbiu isemayo: (kutokana na nuru ya Fatuma -a.s- tunaangaza dunia), wameshiriki zaidi ya wahitimu (1000) kutoka vyuo vikuu (13) vilivyopo kwenye mikoa (12) ya Iraq, kuanzia kaskazini hadi kusini ya nchi, waliosomea bobezi mbalimbali, hafla hii ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa wanawake Fatuma Zaharaa (a.s).
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ammaari Hilliy, ikafuatiwa na kisomo cha surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ulio wasilishwa kwa niaba na mjembe wa kamati kuu na rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi, ameanza kwa kupongeza wahitimu, akasisitiza kuwa kutokana na umuhimu wao tumeona sehemu hii kuwa mahala muwafaka pakufanyia hafla ya kuhitimu kwao, ili kuifanya kuwa kimbilio lao katika Maisha yao kwenye kila jambo lenye maslahi na taifa la Iraq…”.
Kikafuata kiapo cha wahitimu mbele ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha ikasomwa ziara takatifu kwa pamoja na wakahitimisha kwa kusoma Duaau-Faraji ya Imamu wa zama (a.f), halafu wakaenda kumzuru Abulfadhil Abbasi na ndugu yake Imamu Hussein (a.s).
Tunatarajia hafla ya wahitimu itaendelea baada ya Adhuhuri ya leo siku ya Ijumaa, ambapo watakutana na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na kusikiliza ujumbe elikezi kutoka kwake.
Wanafunzi wamefurahi sana kwa tukio hili, wamesema kuwa kufanyika kwa hafla ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kutamka kwao ahadi mbele yake, ni msingi wa mabadiliko katika Maisha yao ya baadae, na watafanya kila wawezalo katika kutumikia taifa hili, wametoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa idara ya shule za Alkafeel za Dini tawi la wanawake kwa kuwaandalia tukio hili tukufu.