Balozi wa Australia nchini Iraq Mheshimiwa Baula Elizabeti ametembelea makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Amepokewa na makamo rais wa makumbusho hiyo Dokta Shauki Mussawi, akifuatana na ujumbe aliokuja nao katika makumbusho hiyo, kuangalia malikale na turathi zilizopo, wamefafanuliwa malengo ya makumbusho na harakati zake, sambamba na kufafanua falsafa ya maonyesho katika makumbusho kwenye sekta tofauti.
Balozi amefurahishwa sana na ziara hii, na amepongeza malikale adimu alizoziona ndani ya makumbusho, akasisitiza kuwa: “Ilikua ni fursa adhim kwake na amefurahia kila alicho kiona katika makumbusho hii yenye historia iliyojaa elimu na mazingatio, akashukuru sana kwa kupewa nafasi hiyo adhim”.
Mwisho wa ziara yake Mheshimiwa Balozi ametoa pongezi na shukrani zake kwa watumishi wote wa makumbusho, kwa mapokezi mazuri na ufafanuzi murua.
Kumbuka kuwa makumbusho ya Alkafeel hupokea wageni mbalimbali kila wakati, kutoka ndani na nje ya Iraq, wanaokuja kuangalia malikale na turathi adimu za kihistoria.