Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imehudhuria na kushiriki kwenye ratiba ya mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa kike wanaosoma kwenye vyuo vikuu na Maahadi.
Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa kike wanaosoma kwenye vyuo vikuu na Maahadi ni moja ya mradi unaosimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu, kwa ajili ya kufikia lengo lililo kusudiwa tumeshiriki kwenye ratiba yao inayo lenga wanafunzi wa kike”.
Akaongeza kuwa: “Ushiriki wetu wa kwanza kwenye mradi huu ulikua wakati wa nadwa ya Qur’ani kwa wanafunzi wa bweni katika chuo kikuu cha Kufa, ambapo mtoa mada alikua ni Sayyid Rashidi Husseiniy aliye ongea kuhusu kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s)”.
Akamaliza kwa kusema: “Maahadi ipo tayali wakati wote kushiriki kwenye kila shughuli inayo husu Qur’ani kwa lengo la kufundisha utamaduni wa Qur’ani, pamoja na kuwa imejikita katika vyuo ambavyo kwa kiwango kikubwa vinachangia kutengeneza mustakbali wa jamii”.
Kumbuka kuwa mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi unahusisha harakati tofauti, miongoni mwa harakati hizo ni: (Kufanya nadwa za Qur’ani ndani ya vitivo na vitengo, pamoja na nadwa kwa wanafunzi wa bweni, kuendesha mashindano ya kuhifadhi Qur’ani na usomaji, maonyesho ya picha za Qur’ani, mashindano ya kuandika Qur’ani, semina za usomaji sahihi wa Qur’ani, na programu za kuendeleza walimu wa vyuo vikuu).