Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanashiriki kwenye uzinduzi wa kukarabati moja ya barabara muhimu inayo elekea kwenye Ataba

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha majengo ya kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wameshiriki katika hatua ya kwanza ya ukarabati wa barabara muhimu inayo elekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Nayo ni barabara ya Jamhuriyya, inaanzia kwenye eneo la Baabu Towareji hadi kwenye makutano ya barabara ya Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambayo ilitengenezwa kipande kidogo siku za nyuma, ikawa barabara ya mfano kutokana na uwezo wake wa kutumiwa na idadi kubwa ya mazuwaru, hususan wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, hasa matembezi ya Towariji ambayo hutumia barabara hiyo.

Kazi hiyo inafanywa na idara ya mitambo na vifaa vya ujenzi pamoja na idara ya ujenzi kwa kushirikisha idara ya mkoa wa Karbala tukufu, chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, ujenzi huo ni pamoja na uchimbaji wa mitaro ya pembeni ya barabara na sehemu za kuweka njia za umeme, nyaya za taa, mawasiliano na mengineyo, hatua ya kwanza inajengwa sehemu yenye urefu wa mita (1200) pembezoni mwa barabara, hatua zingine zitafuata baadae.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa kazi hiyo wanasema kuwa, hatua hii ndio msingi wa mradi wa kukarabati barabara hii muhimu, kwani ndio imebeba sura ya mji wa Karbala na inatunza urithi wa mkoa, na kuufanya mkoa wa Karbala uwe kama unavyotakiwa kuwa sambamba na heshima ya mkoa huu katika nyoyo za waislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: