Kuanza maandalizi ya shindano la Qamarul-Qur’aniyya la kitaifa

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeanza maandalizi ya kufanya shindano la Qamarul-Qur’aniyya la kitaifa la mara ya kwanza, shindano maalum kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari la kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.

Hatua ya kwanza ya Maahadi chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya ni kupanga ratiba ya shindano pamoja na mambo mengine yatakayo fanyika, kisha ikaundwa kamati ya mialiko yenye jukumu la kualika idara za malezi, kamati hiyo imehusisha wawakilishi wa idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule shini ya kitengo cha mahusiano, na wawakilishi wa Maahadi ya Qur’ani.

Tayali idara (20) za malezi kutoka mikoa tofauti, zimesha pewa mialiko pamoja na kukutana na wakuu wa idara hizo, na kuwapa maelezo kamili kuhusu shindano hilo na ratiba yake, ili waweze kuchagua wasomaji wanaofaa kushiriki katika shindano hilo na kuwafanyia maandalizi, hali kadhalika wametembelea wizara ya malezi na kuangalia harakati mbalimbali za kimasomo na kimichezo.

Idara ya malezi imeonyesha utayali wa kushiriki kwenye shindano hilo la Qur’ani, aidha imeshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kufanya harakati hii tukufu inayo Imarisha usomaji wa Qur’ani kwa wanafunzi.

Kumbuka kuwa hili ni moja ya mashindano yanayo simamiwa na Majmaa ya Qur’ani tukufu, sehemu ya shindano hili litafanyika katika mwezi wa (Machi) mwaka huu ndani ya haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kutakua na zawadi kwa washindi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: