Nadwa inatarajiwa kufanywa kwa njia ya mahudhurio ya moja kwa moja na kwa njia ya mtandao kuanzia saa moja jioni siku ya Jumanne (28 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (1 Februari 2022m), mtoa mada atakua ni Dokta Aamir Abdu Zaidi Alwaailiy na Dokta Asadi Abdurazaaq Asadiy mkufunzi katika chuo kikuu cha Alkufa, chini ya uwenyekiti wa Dokta Ammaar Abdurazaaq Swaqhiir.
Mada zilizopangwa na kituo ni hizi zifuatazo:
- - Kuanzishwa kwa jamii yakitaifa na maendeleo yake kihistoria.
- - Mtazamo wa kiislamu kuhusu jamii ya kitaifa.
- - Uwelewa na hali halisi.
Kumbuka kuwa sehemu itakapo fanyika nadwa ni ndani ya ukumbi wa Shekh Answari katika jengo la Imamu Murtadha mjini Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya, karibu na daraja la Thaurah-Ishrina, barabara ya Posta.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao utafanyika kupitia link ifuatayo: zoom https://us02web.zoom.us/j/2646987000