Masomo ya kwanza katika semina ya kusimama na kuanza kwa wanafunzi wa mradi wa Qur’ani Alkafeel

Maoni katika picha
Wanafunzi wa mradi wa Qur’ani Alkafeel, unaosimamiwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kufundishwa masomo ya mwanzo ya kusimama na kuanza katika semina hiyo.

Mkufunzi wa semina ni Dokta Muhammad Abdushakuur ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuhudhuriwa na makumi ya wanafunzi.

Tambua kuwa mradi huo unahusisha masomo ya hukumu za usomaji, tajwidi, naghma, kusimama na kuanza, maarifa ya Qur’ani tukufu na njia za ufundishaji, kila siku ya Alkhamisi saa kumi jioni, na muda wa masomo ni saa mbili mfululizo.

Kumbuka kuwa kusimama na kuanza ni sehemu ya elimu za lugha zinazo husiana na utamkaji sahihi wa maneno ya kiarabu, sambamba na kubainisha malengo ya maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu, na kufahamu maana ya maneno ya Qur’ani takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: