Katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya ametembelea Atabatu Abbasiyya na kukutana na katibu mkuu wake na kumpongeza kwa kupewa madaraka hayo

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu Sayyid Issa Khurasani na ugeni aliofuatana nao, jioni ya leo siku ya Jumatatu wametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, na kupokewa na katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini na makamo wake pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu.

Baada ya wageni kufanya ibada ya ziara na kusoma dua mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakiwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, walikwenda kwenye ukumbi wa utawala na kumpongeza Sayyid Dhiyaau-Dini kwa kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa Ataba takatifu, wakamuomba Mwenyezi Mungu kwa baraka za anayemtumikia amuwezeshe kutumikia malalo hiyo na mazuwaru watukufu, na wakamtakia mafanikio mema katika shughuli zake.

Kikao hicho kilikua na maneno mazuri baina yao pamoja na kujadili namna ya kuboresha ushirikiano baina ya Ataba mbili takatifu Alawiyya na Abbasiyya, na jinsi ya kuboresha huduma kwa mazuwaru watukufu.

Mwisho wa kikao Sayyid Khurasani akaomba dua kwa baraka za mwenye malalo hii takatifu, awawezeshe wasimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kutekeleza majukumu yao ya kuhudumia mazuwaru watukufu, sambamba na kukabidhi bendera ya kubba la malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) kwa Sayyid Mustwafa Dhiyaau-Dini, pamoja na kupeana zawadi za kutabaruku kutoka katika malalo zao takatifu, kisha wageni wakaagwa kwa bashasha kama walivyo karibishwa na kuwaombea kukubaliwa kwa ziara yao na ibada zao na kurudi salama.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: