Kuanza shindano la kuandika Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza kuanza kwa shindano la uandishi wa Qur’ani kwa njia ya mtandao linalo husisha wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi za Iraq waliopo mashuleni.

Shindano linalenga kusambaza utamaduni wa Qur’ani katika jamii ya wanafunzi wa vyuo vikuu, shindano hili ni sehemu ya mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi ambapo wanashiriki kwa njia ya mtandao.

Mashariti ya shindano:

  • - Shindano ni maalum kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo katika vyuo vikuu na Maahadi za Iraq.
  • - Tarehe ya mwisho kupokea majibu ni mwezi (13 Rajabu-Aswabu 1443h).
  • - Mshindi anatakiwa kuambatanisha uthibitisho wa kuendelea kwake na masomo katika chuo au Maahadi wakati wa kupokea zawadi.

Kama washindi wakifungana itapigwa kura ili kupata washindi (15) ambao watapewa zawadi, tambua kuwa shindano linajumla ya maswali (50).

kumbuka kuwa mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi unamambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni: (Kufanya nadwa za Qur’ani ndani ya vitivo na vitengo, pamoja na kufanya nadwa ndani ya mabweni, kuendesha mashindano ya Qur’ani, ya kuhifadhi na kusoma, kufanya maonyesho ya picha za Qur’ani, mashindano ya kuandika Qur’ani, semina za usomaji sahihi wa Qur’ani na kanuni za tajwidi, program ya kuendeleza wakufunzi wa vyuo vikuu).

Kumbuka kuwa mradi unalenga kuhuisha harakati za Qur’ani katika vyuo vikuu na Maahadi, kwa lengo la kukuza vipaji vya vijana wetu watukufu, na kuendeleza vipaji vyao vya kidini na kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: