Kituo cha kiislamu na masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeandaa hafla ya kuwazawadia wakufunzi wa hatua ya kwanza ya semina ya kielimu kuhusu Aqida na fikra za kisasa, ikiwa ni sehemu ya kuthamini juhudi zao wakati wa semina na mafanikio makubwa yanayo tuwezesha kuendelea na hatua ya pili.
Ugawaji wa zawadi umefanywa ndani ya ukumbi wa Shekh Answari katika jengo la Murtadhwa (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mkoa wa Najafu, na kuhudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu Sayyid Liith Mussawi na rais wa kitengo cha Habari na utamaduni Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiriy, pamoja na kundi kubwa la wanachuoni na viongozi wa Dini kutoka hauza na kwenye taasisi za kisekula.
Kando na zowezi la ugawaji wa zawadi imetangazwa hatua ya pili ya semina hii, itakayo fanyika hapa Iraq kwa mara ya kwanza ikiwa na mada mbalimbali, itaendelea hadi mwisho wa mwezi mtukufu wa Shabani.
Hatua ya pili itakua na mihadhara (56), kila wiki kutakua na mihadhara (6) jumla zitakua siku (69) na mada zitakua kama zifuatazo:
Mada ya kwanza: utangulizi wa msingi katika masomo ya Dini: mihadhara 10, itahusisha: (Akili, maumbile, mwanaadamu, maarifa, Dini).
Mada ya pili: mwenendo wa kiislamu: mihadhara 12, itahusisha mada zifuatazo: (mfumo wa kunukuu, mfumo wa misingi, mfumo wa falsafa, mfumo wa maneno, mfumo wa Irfani).
Mada ya tatu: kutojulikana (uhalisi wa kutojulikana) mihadhara 24, itahusu mada zifuatazo: (madiyya na ilmawiyya, ubeberu, uleberali, uchumi wa mitaji, teknolojia, ukoloni, kuvua ubinaadamu, kiwango cha maarifa, akili na desturi).
Mada ya nne: Istishraaq, itakua na mihadhara 10 kuhusu (elimu ya aqida na ushirikina).
Kumbuka kuwa semina hii kwa hatua zake tatu ni miongoni mwa juhudi za kuandaa wasomi wenye uwezo wa kupambana na changamoto za sasa katika elimu ya aqida na mambo ya ushirikina na umagharibi, sambamba na kufundisha Dini halisi, kwa kufanya semina na nadwa mbalimbali kwa makundi yote ya jamii, pamoja na kubaini changamoto za kielimu, kiuchumi na kijamii na kuzitafutua ufumbuzi, sambamba na kuendelea kusaidia miradi ya utafiti ndani na nje ya Iraq.