Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu imefungua moja ya semina za mradi wa Qur’ani katika vyuo vikuu na Maahadi

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefungua semina ya kwanza ya kanuni za tajwidi na usomaji sahihi, ambayo ni sehemu ya mradi wa Qur’ani katika vyuo vikuu na Maahadi.

Kikoa cha ufunguzi kilicho fanywa kwa njia ya mtandao kimehudhuriwa na zaidi ya washiriki (50), semina hii itakua inafanywa siku tatu kwa wiki, chini ya ukufunzi wa Shekh Mahadi Qalandari Albayati, hii ni semina maalumu kwa wakufunzi na watumishi wa chuo, zitafuata semina za wanafunzi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

Mradi wa Qur’ani vyuoni na kwenye Maahadi, unasemina tofauni, mashindano, hafla pamoja na harakati zingine.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu hufanya harakati mbalimbali zinazo husu Qur’ani mwaka mzima.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu kupitia matawi yake yote, ni sehemu ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajukumu la kufundisha Qur’ani na kuandaa jamii inayofanyia kazi mafundisho ya Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: