Idara ya teknolojia na taaluma za mitandao chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa ziara makhasusi ya Imamu Hussein ya mwanzoni mwa mwezi wa Rajabu, ambayo Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Atakae mzuru Hussein (a.s) katika siku ya kwanza ya mwezi wa Rajabu, Mwenyezi Mungu atamsamehe kabisa), hivyo itawafanyia ziara kwa niaba watu wote watakao jisajili kwenye ukurasa wa (ziara kwa niaba).
Ziara hizo zitafanywa na idara ya masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajumuisha pia ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Hali kadhalika kuna ziara ya Imamu Baaqir (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, itakayo fanywa pembeni ya kaburi lake huko Bakii katika mji wa Madina, ziara hiyo itafanywa na kundi la waumini wa kujitolea wanaoishi katika mji wa Mtume (s.a.w.w) Madina.
Kwa kila mtu anayetaka kufanyiwa ziara ajisajili kwenye ukurasa wa (ziara kwa niaba) uliopo kwenye toghuti ya kimataifa Alkafeel kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/