Ataba mbili tukufu zimepokea mwili wa Marjaa-Dini Shekh Swafi Gulbaigani kwa mafuriko makubwa

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Alasiri ya leo siku ya Alkhamisi (1 Rajabu 1443h) sawa na tarehe (3 Februari 2022m), zimepokea mwili mtukufu wa Marjaa-Dini Sheikh Lutfi-Llahi Swafi Gulbaigani aliyefariki siku ya Jumanne iliyopita.

Jeneza lake limeshindikizwa na idadi kubwa ya viongozi wa Dini na wawakilishi wa ofisi za Maraajii-Dini kutoka mji wa Najafu pamoja na wanafunzi wengi wa hauza na waumini kwa ujumla.

Mapokezi hayo yameanzia katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ambapo yameongozwa na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu wake mkuu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini na makamo wake, pamoja na wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo bila kusahau watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Amefanyiwa ibada ya ziara na kusomewa dua mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kisha msafara ukaelekea Atabatu Husseiniyya tukufu, ambako umepokewa na katibu mkuu wake na viongozi wa Ataba hiyo pamoja na watumishi wa malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), ambako amefanyiwa ibada ya ziara kisha akazikwa jirani na malalo ya Imamu Hussein (a.s) na hapo ndio makazi yake ya mwisho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: