Kumbukumbu ya kuzaliwa mwezi wa kumi Imamu Ali bun Muhammad Alhaadi (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi pili Rajabu -kwa mujibu wa riwaya- ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu wa kumi miongoni mwa Maimamu wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), walio takaswa na Mwenyezi Mungu mtukufu, naye ni Imamu Ali bun Muhammad bun Ali bun Mussa bun Jafari bun Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s).

Alizaliwa katika Kijiji cha (Swarya) kipo umbali wa kilometa tatu kutoka Madina, kilianzishwa na babu yake Imamu Mussa bun Jafari (a.s), hakika alikua mfano mwema wa kuigwa katika maadili, zuhudi na elimu, alitumia Maisha yake yote katika kutumikia Dini tukufu, akabanwa sana na watawala wa bani Abbasi, katika zama zake alikutana na utawala wa Mu’taswimu, Waathiqu, Mutawakkil, Muntaswiru, Mustainu na Mu’tazu.

Aliendeleza mafundisho ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w), naye ni miongoni mwa watu wa nyumba ya Mtume kilele cha ubinaadamu na mwisho wa Mitume, baba yake ni Imamu mtakatifu na mama yake ni mama mtukufu bibi Sumana kutoka Moroko.

Imamu Alhaadi (a.s) alizaliwa na kulelewa chini ya uongofu wa Qur’ani tukufu na tabia za Mtume (s.a.w.w) alizopambika nazo baba yake mtukufu, alama za utukufu wake zilionekana mapema kama ishara ya kuteuliwa kwake na Mwenyezi Mungu tangu akiwa mdogo.

Imamu Alhadi (a.s) amepambika kwa tabia njema alizokuwa nazo babu yake Mtume mtukufu, hakika alikua na kila aina ya tabia nzuri, nafasi haitoshi kueleza kila kitu.

Alichukua madaraka ya Uimamu baada ya baba yake akiwa na umri wa miaka nane, Maisha ya Imamu huyu yamegawanyika sehemu mbili kubwa: sehemu ya kwanza ni miaka aliyo ishi na baba yake Imamu Jawadi (a.s), nayo ni chini ya muongo mmoja (miaka kumi), na sehemu ya pili ni zaidi ya miongo mitatu, ndani ya kipindi hicho alishuhudia watawala sita wa bani Abbasi, ambao ni: Mu’taswimu, Waathiqu, Mutawakkil, Muntaswiru, Mustainu na Mu’tazu.

Mutawakkil alikuwa sawa na watawala waliotangulia katika kuamiliana na Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s), bali yeye alimwita Imamu Alhadi (a.s) katika jumba la utawala huko Samaraa na akamtenga na umma wake.

Pamoja na kumtenga na umma alimuweka kizuwizini chini ya ulinzi mkali katika mji wa Samaraa, lakini Imamu aliendelea kutekeleza wajibu wake kwa umakini na tahadhari, aliendelea kufundisha na kulea wanachuoni kupitia misafara ya waislamu waliokua wakimtembelea.

Amani iwe juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyokufa na siku atakayo fufuliwa kuwa hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: