Idara ya Qur’ani inaendelea na ratiba yake ya (Ulizeni wajuao)

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani kwa kushirikiana na idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea na ratiba ya (Ulizeni wajuao).

Ratiba hiyo inahusu kusoma juzuu la thelathini la Qur’ani kila wiki kwa njia ya mtandao chini ya anuani isemayo (Basi na watafakari aya zake).

Ratiba imejaribu kuangazia Maisha ya Imamu Alhaadi (a.s), zimeimbwa kaswida za kuonyesha mapenzi kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), sambamba na kutoa mafundisho maalum kwa watoto.

Aidha Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) imeshuhudia mahudhurio makubwa ya wanafunzi wa madrasa ya Zaharaa (a.s) pamoja na wanafunzi wa madrasat Fatuma bint Asadi (a.s) na kundi la mazuwaru watukufu.

Ratiba imehitimishwa kwa kufanya mashindano na kutoa zawadi kwa washindi, kisha watu wote wakasimama na kusoma Duau-Faraji ya Imamu wa zama (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: