Kufanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alhaadi (a.s) ndani ya ukumbi wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali Alhaadi (a.s), chini ya ratiba ya kuomboleza iliyo andaliwa.

Majlisi imeratibiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu na itaendelea kwa muda wa siku tatu, kuanzia siku ya Ijumaa Mwezi pili Rajabu hadi mwezi nne, kila siku itafanyika mara mbili asubuhi na jioni.

Kiongozi wa idara hiyo Shekh Abduswahibu Twaiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Majlisi hizi ni sehemu ya mradi wa Ummul-Banina (a.s) wa kitablighi, wa kufanya na kuratibu shughuli za uombolezaji ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu, hufanywa kila mwaka mara mbili kwa siku, asubuhi chini ya uhadhiri wa Shekhe Dhiyaau-Al-Abadi na jioni anazungumza shekhe Ridhwa Twawirijawi, pamoja na kufanya majlisi ya (matam), inayo ongozwa na muimbaji Haidari Saadi na Ali Waaili Karbalai”.

Akaongeza kuwa: “Mihadhara iliyotolewa imeangazia historia ya Imamu Alhaadi (a.s), chini ya ratiba iliyo andaliwa, kila mhadhiri ameongea mada tofauti na mwenzake”.

Akafafanua kuwa: “Wameangazia historia ya Imamu Alhaadi (a.s), na changamoto alizopata katika Maisha yake kutoka kwa watawala, na vipi alifanikiwa kufikisha ujumbe wa Dini tukufu ya kiislamu na mwenendo wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) pamoja na changamoto zote alizo kutana nazo”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya kuomboleza yenye vipengele vingi, kwa mfano utoaji wa mihadhara ya kidini, kufanya majlisi za kuomboleza na kupokea mawakibu za waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: