Huzuni katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Alhaadi (a.s): Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi ya kuashiria msiba

Maoni katika picha
Huzuni imetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuta zake zimewekwa mapambo meusi kama ishara ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali Alhadi (a.s), ambaye alikufa tarehe kama ya leo siku ya Jumamosi mwezi tatu Rajabu-Aswabu.

Bendera za kuonyesha ishara ya kuomboleza zimepandishwa na taa nyekundu zimewashwa, vitambaa ambavyo vimeandikwa maneno yanayo ashiria kuomboleza vimewekwa ndani ya ukumbi wa haram tukufu, kama sehemu ya kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) kwa msiba huu.

Kutokana na tukio hilo Atabatu Abbasiyya tukufu -kama kawaida yake- imeandaa ratiba ya kuomboleza yenye vipengele vingi, kama utoaji wa mihadhara ya kidini, kufanya majlisi za kuomboleza pamoja na kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa utawala, na kufanya matembezi ya maukibu ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Hali kadhalika kitengo cha Habari kimeandaa vipindi maalum vitakavyo rushwa kwenye vyombe vya Habari kupitia masafa ya bure, sambamba na hayo Ataba tukufu imetoa magari mengi kwa ajili ya kubeba waombolezaji kutola Karbala hadi Samaraa, kwenda kusaidia watumishi wa Atabatu Askariyya katika kuhudumia mazuwaru watukufu.

Kitengo cha mawakibu nacho kimeandaa utaratibu maalum wa kupokea mawakibu za waombolezaji katika Ataba mbili tukufu, pamoja na mkakati wa kutoa huduma, na idara ya wanawake pia imeandaa ratiba maalum yenye vipengele vingi.

Aidha mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu umejipanga kugawa mamia ya sahani za chakula kwa waombolezaji.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu -kama kawaida yake- imeandaa ratiba ya uombolezaji yenye vipengele vingi, kama vile kutoa mihadhara ya kidini, kufanya majlisi za kuomboleza na kupokea mawakibu za waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: