Mawakibu za kutoka Karbala zinaomboleza kifo cha Imamu Alhaadi (a.s)

Maoni katika picha
Mawakibu za Karbala tangu asubuhi ya leo mwezi (3 Rajabu 1443h) sawa na tarehe (5 Februari 2022m) zimekua zikimiminika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kuhuisha na kuomboleza kifo cha Imamu Ali Alhaadi (a.s) na kuwapa pole Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wapenzi wao kufuatia msiba huu uliotokea mwaka wa 254h.

Matembezi ya uombolezaji yalianzia kwenye barabara ya Saaqi Atwasha Karbalai (a.s), huku wakiimba kaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni.

Kisha matembezi hayo yakaelekea upande wa mlango wa Imamu Hassan (a.s) katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakipiga matam, hadi wakafika katika hara ya Imamu Hussein na wakafanya majlisi ya kuomboleza Jirani na malalo ya baba wa Maimamu (a.s).

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya -kama kawaida yake- imeandaa ratiba ya kuomboleza yenye vipengele vingi, kama vile utoaji wa mihadhara ya kidini, kufanya majlisi za kuomboleza na kupokea mawakibu za waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: