Maukibu ya watumishi wa Ataba mbili tukufu inahuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Alhadi (a.s)

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya Jumamosi mwezi (3 Rajabu-Aswabu 1443h), yamefanywa matembezi ya maukibu ya pamoja ya wahudumu wa Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya, imekwenda kutoa pole kwa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kukumbuka kifo cha Imamu Ali Alhadi (a.s).

Matembezi yameanzia ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha waombolezaji wakaelekea kwenye malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, huku wakiimba kaswida za huzuni na majonzi kufuatia kifo cha Imamu wa kumu (a.s).

Baada ya kuwasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s) wakafanya majlisi ya kuomboleza, ambapo wameimba pia kaswida na kusoma tenzi zilizo amsha hisia ya huzuni katika nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Kumbuka kuwa mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, zimekua zikiwasili tangu asubuhi ya leo katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kuja kuwapa pole, pamoja na Imamu wa zama (a.f) kutokana na msiba huu mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: