Atabatu Askariyya tukufu imepokea makundi ya waombolezaji kutoka mikoa tofauti ya Iraq na nchi tofauti, yaliyokuja kumpa pole Imamu wa zama (a.f) kwa kifo cha babu yake Imamu Ali Alhadi (a.s).
Chini ya utaratibu maalum ulio wekwa na Ataba tukufu na wasaidizi wao kutoka Ataba zingine za hapa Iraq, vikundi vya watoa huduma vimeenea kwenye barabara zote zinakwenda kwenye haram tukufu, mawakibu kutoka sehemu mbalimbali zimekuja kuhudumia mazuwaru kwa kugawa chakula, vinywaji, malazi pamoja na huduma zingine za kibinaadamu.
Kumbuka kuwa tangu siku za nyuma Atabatu Askariyya imekua ikishuhudia makundi ya watu yakija kufanya ziara kwa wingi kutokana na kuwepo kwa matukio mawili, tukio la kuzaliwa kwa Imamu Alhaadi (a.s) -kwa mujibu wa riwaya-, aliyezaliwa tarehe mbili Rajabu-Aswabu, na mwezi tatu Rajabu ni kumbukumbu ya msiba wa kifo chake (a.s), kilele cha waombolezaji ni leo mchana baada ya Adhuhuri.