Masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya wamefanya ziara ya Imamu Ali Alhaadi (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake mbele ya kaburi lake takatifu katika mji wa Samaraa kwa niaba ya maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya Iraq walio jisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba uliopo katika mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu (mtandao wa kimataifa Alkafeel).
Kiongozi wa idara ya masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Hashim Shami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumefanya ziara kwa niaba ya kila aliyejisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba, idadi ya watu wanaojisajili kwenye ukurasa huo inaongezeka siku baada ya siku”.
Akaongeza kuwa: “Tulikuwepo katika malalo ya maimamu wawili Askariyaini (a.s) huko Samaraa, tumefanya ziara mara nyingi, ambazo ni ziara maalum na zisizokua maalum pamoja na swala za suna ya ziara, sambamba na kusoma dua na Qur’ani na kuelekeza thawabu zake kwa wale waliojisajili”.
Akafafanua kuwa: “Hatukuwasahau wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) mashariki na magharibi ya dunia katika kuwaombea wapate afya na amani kwa baraka ya tunaemkumbuka”.
Kumbuka kuwa ukurasa wa ziara kwa niaba hutembelewa na watu wengi katika mtandao wa kimataifa Alkafeel, ni kiunganishi kikubwa kati ya mazuwaru na malalo za maimamu na familia zao takatifu (a.s) ndani na nje ya Iraq, zaidi ya watu milioni tano (5,000,000) wamejisajili.