Kituo cha kuhuisha turathi kimetoa nakala iliyohakikiwa kuhusu uongo aliozushiwa Aqiil bun Abu Twalibu

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha kuhuisha turathi katika maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kitengo cha Habari na utamaduni, kimetoa kitabu kilicho hakikiwa kwa anuani isemayo: (Aqiil bun Abu Twalib ni alama ya nasaba mashuhuri), kilichoandikwa na Shekh Abdulwahidi Mudhwafar aliyekufa mwaka 1395h.

Kitabu kina juzuu (120) zote zimehakikiwa na kituo, kupitia nakala halisi zilizo andikwa na muandishi kwa hati nzuri na umaridadi mkubwa.

Mkuu wa kituo Ustadh Muhammad Wakili ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Umma wetu wa kiislamu unamtihani wa kuwepo kwa baadhi ya kalamu za kulipwa, zisizo andika ukweli, na zimefuata mlengo wa waliohalifu maelekezo ya kitabu kuhusu uhalifa wa Abu Turaab, hivyo ni lazima kwa waandishi wakweli kuondoa wingu la uzushi na kubainisha ukweli, na kuonyesha uongo ulioingizwa kwenye historia, miongoni mwa vitabu vinavyo fichua ukweli ni hiki”.

Akaongeza kuwa: Muandishi wa kitabu hiki Shekhe Abdulwahid Mudhwafar ameonyesha uongo aliozushiwa Aqiil bun Abu Twalib, kwa kuandika historia yake kwa mtindo ufuatao:

 • - Kubainisha nasabu ya Aqiil.
 • - Kutaja mwaka aliozaliwa na kueleza makuzi yake.
 • - Kubaini wakati waliosilimu.
 • - Kutaja kuhama kwake Makka na wakati aliohama.
 • - Majina la kuniya, lakabu, sifa, ushujaa na ushiriki wake katika vita bamoja na Mtume, na nafasi yake katika kuhami ujumbe aliokuja nao Mtume wa Mwenyezi Mungu.
 • - Nafasi yake mbele ya Mtume na jinsi alivyokua anampenda.
 • - Maarifa yake na elimu mbalimbali.
 • - Kulinda Dini yake na itikadi yake.
 • - Kuweka mapungufu katika mambo yanayo muhusu Aqiil na sababu zake,
 • - Sifa za wanachuoni kwa Aqiil na rai zao kwake,
 • - Kutaja kifo chake na sehemu lilipo kaburi lahe.

Kumnuka kuwa kitabu hiki ni moja ya vitabu vilivyo hakikiwa na kituo na kuandikwa katika muonekano mpya, jambo hilo linatokana na maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya kuhakiki nakala kale na vitabu visivyo hakikiwa, kisha kuchapishwa katika muonekano mpya baada ya kuhakikiwa na jopo la wanachuoni waliobobea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: