Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imeshiriki kwenye mradi wa vituo vya Qur’ani kwa kufundisha usomaji wa Qur’ani sahihi kwa mazuwaru wa Maimamu wawili Askariyaini (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Alhadi.
Imeshirikiana na Atabatu Askariyya tukufu, vilifunguliwa vituo kadhaa katika barabara zinazo elekea kwenye malalo takatifu, kwa ajili ya kulenga makundi ya watu wanaokwenda kufanya ziara, zaidi ya walimu (25) wameshiriki kenye mradi huo.
Vituo hivyo vilikua na jukumu la kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani, hususan sura ambazo husomwa mara nyingi katika swala, kujibu maswali na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa mazuwaru, sambamba na kutoa vipeperushi vinavyo elezea ziara na mambo mengine yanayo husu Qur’ani.
Takumbua kuwa ushiriki huu upo chini ya ratiba ya Maahadi ya Qur’ani inayolenga kufundisha Qur’ani kwa jamii.
Vituo vimepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru hasa wasiokua waarabu, wameshukuru na kupongeza mradi huu muhimu wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani na nyeradi za swala, jambo ambalo ndio sharti la kuswihi faradhi hiyo tukufu.